Bodi ya maji bonde la wami/ruvu kupitia wizara ya maji na mfuko wa fedha kutoka shirika la kimataifa la maendeleo (UNDP) na mfuko wa mazingira wa dunia (GEF, inatekeleza mradi wa kunusuru vyanzo vya maji kupitia matumizi bora ya ardhi katika kidaka maji cha Ruvu (Kielelezo). Mradi huu wa miaka mitano (2016 – 2020) unatekelezwa katika kidakio cha Ruvu mkoani Morogoro na Zigi mkoani Tanga.