Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ametembelea Banda la Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu kwenye maonesho ya Wiki ya Mazingira Duniani ambayo kilele chake ni leo Juni 05,2021, ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Phillip Mpango ndio alifunga maonesho hayo katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Dodoma.  Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu imeshiriki Wiki ya Mazingira Duniani, kwa kutoa elimu ya utunzaji wa Rasilimali za Maji