Bodi ya Maji Bonde la Mto Wami/Ruvu imetoa mashine za kufyatulia matofali ya Interlock kwa Jumuiya ya watumia maji ya Mgeta Juu A mkoani Morogoro.

Mashine hiyo zimetolewa kupitia mradi wa uendelezaji wa sekta ya maji awamu ya pili (Water Sector Supporting project WSSP 11) na kupitia mashine hiyo itawawezesha wanajumuiya hao kufyatua tofali za kujenga Ofisi yao pamoja na kuwa chanzo cha mapato kitakachowawezesha kupata fedha kwa ajili ya kujiendesha na usimamizi wa Rasilimali za Maji katika eneo hilo.