Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Phillip Mpango akiwasili katika Viwanja vya Ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Mjini Dodoma.

Dkt Mpango anahudhuria kilele cha Wiki ya mazingira Duniani, ambapo Bodi ya maji katika Bonde la Wami Ruvu inashiriki kwa lengo la kutoa Elimu kwa Wananchi kuhusiana na majukumu yake na umuhimu wa kutunza na kuhifadhi vyanzo vya maji kwenye Visima, mito na mabwawa.