Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri ametembelea eneo la hifadhi ya maji chini ya ardhi Bonde la Makutupora na kukagua shuguli za uhifadhi wa chanzo hicho ikiwa ni pamoja na uchongaji wa njia za kuzuia moto (fire break) zenye urefu wa zaidi ya  kilomita 91, uwekaji wa alama za mipaka na mabango ya kudumu  kuonyesha mwanzo na mwisho wa hifadhi.

Mhe. Shekimweri ameridhiswa na kazi kubwa inayoendelea kufanywa na Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu ya kulinda na kulihifadhi bonde hilo ambalo ndio chanzo kikuu cha maji kinachotegemewa na wakazi wa Dododoma huku akiwataka wananchi kuachana kabisa na shughuli mbalimbali za kibinaadamu zinazosababisha milipuko ya moto kaika eneo hilo ikiwa ni uchomaji wa mkaa n.k