- Kufanya vipimo vya mtiririko wa maji juu ya ardhi na Matukio ya mkondo (Mafuriko na ukame) na mahitaji maalum
- Kukusanya, kuchakata, kuchambua takwimu na kuhifadhi kumbukumbu kwa ajili ya usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji. Tunakusanya takwimu za hali ya hewa, kiwango cha maji na ubora wa Maji
- Kutathmini, kutunza na kuhuisha takwimu na taarifa kuhusu upatikanaji na mahitaji ya rasilimali za maji
- Tunajenga na kufanya matengenezo ya mitandao ya Kihaidrolojia na Hali ya Hewa
- Kuainisha vyanzo vya maji kwa maendeleo
- Kurejesha hali asili ya vyanzo, kutathmini na kupanga mipango ya utunzaji wa Mito
- Kutoa taarifa ya mtiririko wa maji, mahitaji ya maji na kutoa onyo la mapema la mabadiliko ya hali ya hewa (mafuriko na ukame) ndani ya bondeĀ
- Kufanya uhakiki wa ubora na udhibiti wa takwimu za kihaidrolojia
- Kutambua maeneo yanayowezekana, kubaini, kuandaa kwa kujenga mabwawa