Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu Mhandisi Elibariki Mmassy akiwa kwenye mahojiano maalumu na TBC ambapo ametoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira haswa uhifadhi wa bonde la makutupora ambalo ndio chanzo pekee cha maji kwa jiji la Dodoma.
Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu inaendelea na zoezi la Uchongaji wa njia za kuzuia moto (fire break) katika hifadhi ya maji bonde la Mkutupora Dodoma
Zoezi la Uwekaji wa alama za mipaka na mabango ya kuzuia shughuli za kibinaadamu ndani ya hifadhi ya bonde la Makutupora Mkoani Dodoma
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akizindua Mradi wa Huduma ya Maji na Birika la Kunyweshea Mifugo Katika Kijiji cha Ruvu Darajani Uliogharimu Kiasi cha Shilingi Millioni 65 ambao utanufaisha Zaidi ya Mifugo 2000 kunywa maji kwa siku pamoja na kutoa huduma ya maji safi kwa wakazi wa vijiji jirani vinavozungukwa na Mradi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru 2023 Ndugu. Abdallah Sahib Kaimu amekagua na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa utunzaji wa vyanzo vya maji Tangeni uliopo katika wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.
Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu ina jukumu la kulinda, kutunza na kuhifadhi Rasilimali za maji na Mazingira kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji Namba 11 ya Mwaka 2009. Katika kutekeleza sheria hii ya kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji.