Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru 2023 Ndugu. Abdallah Sahib Kaimu amekagua na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa utunzaji wa vyanzo vya maji Tangeni uliopo katika wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro wenye thamani ya shilingi Bilioni 13 ambapo lengo la mradi huu likiwa ni kutunza mazingira ili kuhimili mabadiliko ya tabia nchini.

Akikagua Mradi huo Ndugu Abdallah Shaib ameipongeza Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu kwa utekelezaji wa mradi huo kwa kuweka alama za mipaka ya mita 60, uwekaji wa mabango ya makatazo Pamoja na kuweka uzio ili kuzuia uchafuzi unaoweza kufanyika na kuharibu mazingira Pamoja na ubora wa maji kiujumla.

Mradi huu umekuwa ni mingoni mwa miradi inayoendana na kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2023 inayosema “Tunza mazingira, Okoa vyanzo vya maji, kwa ustawi wa viumbe hai na uchumi wa Taifa”