Bodi ya maji Bonde la Wami/ Ruvu ilianzishwa julai 2002 kwa mujibu wa sheria Na. 11 ya mwaka 2009 (iliyofuta sheria Na. 42 ya mwaka 1974 na marekebisho yake) nchi nzima imegawanywa katika mabonde makuu tisa (9). Bodi ya maji bonde la wami/ ruvu ina ofisi tat una makao makuu yako Morogoro mjini na ofisi ndogo ziko Dodoma na Dar es salaam. Bonde linajuuisha sehemu za mikoa ya Dodoma, manyara, Morogoro, pwani, tanga na mkoa wote wa dar es salaam likiwa na jumla ya wilaya 22 za mikoa hiyo. Bonde linakadiriwa kuwa na kilometa za mraba 66,820 huku eneo la mto wami likiwa na kilometa za mraba 43,946 na eneo la mto ruvu likiwa na kilometa za mraba 18,078 na eneo la bonde la mito ya mpiji, mlalakuwa, msimbazi,kizinga,mzinga na mbezi lkiwa na kilometa za mraba 4,796.

Below is the location of Basin Head Office in Morogoro.