Katika kuendeleza kampani ya Upandaji miti pembezoni mwa vyanzo vya maji, Watumishi kutoka Bodi ya maji Bonde la Wami/Ruvu wamepanda miti pembezoni mwa chanzo cha Mto Mlali ikiwa ni moja ya njia Bora ya utunzaji endelevu wa vyanzo vya maji.

Zoezi hilo lilihudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo watumishi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira Morowasa, jumuiya ya Watumia maji kidakio cha ngerengere juu B pamoja na wananchi wa wilaya ya Mvomero 

Aidha Afisa misitu kutoka Bodi ya maji Bonde la Wami/ Ruvu Emmanuel Komba amesema kuwa zoezi hilo ni endelevu na mpaka sasa wamefanikiwa kupanda miti zaidi ya 500 katika chanzo cha Mto Mlali. Naye Mkuu wa idara ya Mazingira kutoka Mamlaka ya maji Safi na usafi wa Mazingira Mhandisi Rashid Bumarwa amesema kuwa upandaji wa miti utasaidia sana katika utunzaji wa rasilimali hasa katika kupindi cha ukame. 

Kwa upande wao wanachi pamoja na viongozi wa Jumuiya  ya watumia maji wamesema kuwa wamepongezwa na jitihada za Bodi kwa kwenda kupanda miti katika eneo jambo ambalo litapunguza adha ya maji katika kipindi cha ukame kwa wakazi wa eneo hilo pamoja na kuelezea faida za upandaji miti kiujumla.