Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imefanya  kikao na wajumbe wa Shirikisho la viwanda  (CTI) kwa lengo la kujadili maendeleo na changamoto zilizobainishwa katika zoezi la ukusanyaji wa ada za matumizi ya maji ikiwa ni pamoja na baadhi ya viwanda kuficha takwimu sahihi za matumizi ya maji.

 Kikao hiki kimefanyika Jijini Dar es salaam ambapo Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu Bw. Hussein Sufian amesema kuwa  Bodi pamoja na shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) wamekubaliana kushirikiana kikamilifu katika suala la utunzaji wa Rasimali za maji pamoja na kulipia ada za matumizi ya  maji kwa wakati ili kutokwamisha shughuli za uhifadhi wa vyanzo.

Awali akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi kutoka Shirikisho la Viwanda Tanzania Bi. Anna Kimaro  amebainisha kuwa wapo tayari kushirikiana na Wami/Ruvu kwa Maendeleo ya Rasilimali za Maji Nchini.