UTARATIBU WA KUOMBA KIBALI CHA KUTUMIA MAJI JUU NA CHINI YA ARDHI

  1. Barua ya maombi
  2. Mwombaji anatakiwa kujaza fomu ya maombi na kuwasilisha katika ofisi ya Bonde (Morogoro, Dar es Salaam au Dodoma) ikiambatana na ada ya maombi. Ombi husika, ada hizi hutofautiana kutokana na aina ya matumizi ya maji.
  3. Ombi hutangazwa kwenye gazeti la serikali na tangazo hilo huwekwa kwenye mbao za matangazo kwa wakuu wa wilaya husika. Bodi itaomba maoni kutoka kwa watumiaji wa chanzo hicho ambapo wanaweza kuathirika kama ombi litakubaliwa. Pia itaomba maoni kutoka Halmashauri husika. Kwa miradi mikubwa hadi uthibitisho wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) huitajika kwa ajili ya athari za kimazingira na kijamii.
  4. Ofisi kukagua eneo la chanzo cha kuchukulia maji na kuchukua sampuli ili kujua ubora wa maji hayo.
  5. Kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji Na. 11 ya mwaka 2009, baada ya siku arobaini kupita tangu kuombwa kwa maoni na kutangazwa kwenye gazeti la serikali, ombi linaweza kufikishwa katika kikao cha bodi ya maji ya Bonde.
  6. Kibali hutolewa kwa maombi yaliyoidhinishwa na kikao cha bodi. Afisa wa maji ambaye pia ni katibu wa bodi ya maji ya Bonde anaweza kutoa au kutotoa kibali kufuatana na maelekezo ya bodi.
  7. Kwa maombi yaliyokataliwa, waombaji wana haki ya kukata rufaa kwa waziri mwenye dhamana na maji.        

VIAMBATANISHI
Fika ofisi za Ubungo Maji na utajaza form kulingana na ombi unalohitaji, aina ya “form” za maombi ya vibali ikiambatanishwa na taarifa zifuatazo: - 

A. MAOMBI YA KIBALI CHA MATUMIZI YA MAJI (APPLICATION FOR WATER USE PERMIT)

  1. Barua ya maombi 
  2. Ripoti ya uchimbaji kisima, ikionyesha kina (urefu wa kisima) na uwezo wa kisima.
  3. Ripoti ya uchuguzi wa maji juu ya ardhi (Hydrological Survey Report)
  4. Ripoti ya maabara, ikionyesha “ubora wa maji”

B. MAOMBI YA KUTIRIRISHA MAJITAKA (APPLICATION FOR PERMIT TO DISCHARGE)

  1. Barua ya Maombi 
  2. Ripoti ya maabara, ikionyesha kiwango cha maji yanayotupwa (Laboratory Report)  
  3. Leseni ya biashara (Business Licence)
  4. Leseni ya makazi (Licence of Occupancy/Title Deed)
  5. Kibali cha ujenzi (Building Permit)
  6. Kibali cha uzalishaji (Production Permit)
  7. Kiwango cha uzalishaji (Industry Production Capacity)
  8. Environmental Clearance Certificate 
  9. Environmental Audit Certificate 
  10. Final Environmental Audit Report 


C. MAOMBI YA KUCHIMBA KISIMA (APPLICATION FOR PERMIT TO SINK OR ENLARGE A WELL OR BOREHOLE)

  1. Ripoti ya Survey (Survey Report)

D. KUOMBA HAKI YA NJIA KATIKA ARDHI (APPLICATION FOR PERMIT FOR AN EASEMENT)

  1. Kibali cha matumizi ya maji 
  2. Vielelezo vya ardhi ambapo kibali kipo
  3. Vielelezo vya ardhi ambapo maji yanakwenda
  4. Maelezo ya uhamishaji wa maji na kazi zitakazofanyika
  5. Makabrasha/vielelezo vya fidia
  6. Makubaliano ya pande zote mbili